Mwanzo / Website Za Biashara

Website Za Biashara

Weka huduma, bidhaa na mawasiliano ya biashara yako kwenye website inayoeleweka kwa simu na computer. Tunahudumia biashara Tanzania na tunajadili miradi ya kimataifa kwa njia ya mtandao.

Pata Quotation ya Mradi Wako

Tatizo Tunaloangalia

Mteja akikutafuta, asiishie kwenye taarifa zilizotawanyika kwenye posts. Website iwe sehemu moja ya kujua unachofanya, eneo unalohudumia na jinsi ya kuwasiliana nawe.

Kazi Inayoweza Kujumuishwa

Kurasa za huduma, kuhusu biashara na mawasiliano; mpangilio wa simu; links za WhatsApp; na muundo wa content wenye headings zinazoeleweka. Catalog au forms zinajadiliwa kulingana na mradi.

Taarifa Tunazohitaji

Leta logo, huduma, mawasiliano na picha unazoruhusiwa kutumia. Ikiwa maandishi au picha haziko tayari, tutaeleza msaada unaohitajika kwenye quotation.

Hatua Za Kazi

Tunaelewa lengo na kurasa, tunakubaliana scope na gharama, tunaandaa preview, kisha unapitia na kuidhinisha launch na handover.

Mipaka Ya Scope

Domain, hosting, uandishi wa content na integrations zitaonyeshwa kama zimejumuishwa au zinahitaji gharama tofauti. Hakuna ahadi ya nafasi Google au idadi ya mauzo.

Maswali Ya Mara Kwa Mara

Nahitaji kurasa ngapi?

Tutapanga kurasa kutokana na huduma na taarifa zako; si lazima kuanza na website kubwa.

Website itakuwa yangu?

Quotation itaeleza files, accounts, access na majukumu ya domain na hosting kabla ya kuanza.

Huduma Nyingine

Pata Quotation ya Mradi Wako

Kazi, gharama na muda vinakubaliwa kabla ya kuanza.

HATUA INAYOFUATA

Kagua Ombi. Chagua Njia Ya Kutuma.

Pitia maelezo yako hapa chini. Ukiwa tayari, fungua WhatsApp au email na utume ujumbe. Bado hatujapokea ombi hili.

Endelea WhatsAppFungua email