Faragha
Questionnaire ya quotation
Jina, biashara, nchi, industry, features, content, ratiba na mawasiliano vinatumika kuandaa ombi ndani ya browser yako. Majibu hayahifadhiwi kwenye database wala localStorage. Draft huhifadhiwa kwenye sessionStorage ya tab kwa hadi dakika 30 ili kuendelea kati ya kurasa. Kufunga tab huiondoa. Kukagua ombi hakulitumi kwa server.
WhatsApp, email na kunakili
Ukichagua WhatsApp, maelezo ya mradi yanawekwa kwenye link ya wa.me/255652505000. Email au simu uliyojaza haiongezwi kwenye WhatsApp link; WhatsApp inaweza kuonyesha utambulisho wa akaunti yako kwa mpokeaji. Ukichagua email, draft yenye mawasiliano yako hufunguliwa kwa nickson@mastaos.com. WhatsApp/Meta au email provider wanaweza kuchakata taarifa unapofungua app. Wewe unaamua kutuma; kufungua au kunakili si uthibitisho wa kupokea ombi. Kunakili huweka ombi kwenye clipboard yako.
Uthibitisho wa mawasiliano
Form hukagua muundo wa email au namba na kukuomba uhakikishe usahihi. Huu si uthibitisho wa umiliki; hakuna OTP inayotumwa. Umiliki utathibitishwa kupitia mawasiliano yetu baadaye.
Epuka taarifa nyeti
Usiweke passwords, taarifa za kadi, nyaraka za utambulisho au taarifa nyeti kwenye ombi la mwanzo. Taarifa zinazohitajika baadaye zitajadiliwa kwa njia inayofaa.
Lugha na hosting
Lugha ya interface inaweza kuhifadhiwa kwenye localStorage. Questionnaire haitumii GPS wala eneo la ziara kuamua bei. Hosting provider anaweza kuchakata IP na technical logs kwa kuendesha na kulinda huduma. Hakuna advertising pixels au third-party analytics scripts.
Mawasiliano
Ukituma ujumbe, tutautumia kujibu, kupitia mahitaji na kuandaa quotation. Kwa maswali au ombi la kufuta mawasiliano, andika nickson@mastaos.com.
Rudi kwenye quotation