Website Inayoieleza Biashara Yako

Tunakutengenezea website yenye huduma, bidhaa na mawasiliano yako. Mteja aone unachotoa, apate taarifa anazohitaji na aweze kukufikia kwa urahisi, kwenye simu au computer.

Tuambie unachohitaji. Tutakubaliana kuhusu kazi, gharama na muda kabla ya kuanza. Kuomba quotation ni bila wajibu wa kununua.

01 / WEBSITE YENYE KAZI

Wateja Wapate Taarifa Wanazohitaji

Badala ya kutuma picha na maelezo yale yale kila unapoombwa, unaweza kumtumia mteja link moja yenye taarifa za biashara yako.

01

Aelewe Huduma Zako

Weka maelezo ya huduma zako na jinsi ya kuzipata, ili mteja ajue kama unaweza kumsaidia.

02

Aone Bidhaa Au Menu

Onyesha bidhaa, vyumba au menu yako kwa picha na maelezo yanayomsaidia mteja kuchagua.

03

Awasiliane Kwa Urahisi

Mteja akitaka kuuliza au kuagiza, apate WhatsApp, simu au email yako bila kuhangaika.

KWA BIASHARA ZA HUDUMA, BIDHAA NA UKARIMU
Restaurant/CaféUtalii/UsafiriHoteli/MalaziRejareja/BidhaaHuduma za kitaalamuUjenzi/MajengoElimu/MafunzoUrembo/UstawiLogistics/UsafirishajiNyingine
02 / ONA INAVYOFANYA KAZI

Ona Mfano Wa Website Ya Restaurant

Pitia menu, chagua aina ya chakula na ujaribu button ya kuulizia. Ni mfano wa namna website yako inaweza kuonyesha bidhaa au huduma zako.

Jaribu Demo ya Restaurant ↗

Hii ni demo ya biashara ya kubuni, si kazi au testimonial ya mteja. Hakuna oda wala malipo yanayopokelewa.

KIJANI KITCHEN · DEMO

Menu Ya Kijani Kitchen

Menu · Categories · Mawasiliano

MFANO UNAOWEZA KUJARIBU ↗
03 / MRADI WAKO

Quotation Kulingana Na Mahitaji Yako

Huenda unahitaji kurasa chache za huduma, catalog ya bidhaa au mfumo wa booking. Tutaangalia unachohitaji, kisha tukuandalie quotation yenye kazi na gharama zake.

Quotation Yako Itaeleza Nini?

  • Kurasa na features zinazohitajika.
  • Content uliyonayo na msaada unaohitaji.
  • Kazi iliyojumuishwa, isiyojumuishwa na marekebisho.
  • Gharama, ratiba, hatua za malipo na handover.
Pata Quotation ya Mradi Wako
04 / HATUA ZILIZO WAZI

Jinsi Tutakavyofanya Kazi

Tutawasiliana kuhusu mahitaji yako na kukutumia link ya kuona website wakati inaandaliwa. Huhitaji kufika ofisini ili tufanye kazi pamoja.

  1. 01

    Tuambie Mahitaji

    Tuambie kuhusu biashara yako, unachohitaji na taarifa ulizonazo. Unaweza kueleza kwa maneno yako.

  2. 02

    Kubali Scope Na Gharama

    Utapitia quotation yenye kazi tutakayofanya, gharama, muda na utaratibu wa malipo.

  3. 03

    Pitia Website Yako

    Tutakutumia website uipitie na utoe maoni. Marekebisho yatafuata kazi tuliyokubaliana.

  4. 04

    Idhinisha Launch Na Handover

    Ukiridhia kazi na hatua za malipo kukamilika, tunaifungua website na kukupatia maelekezo ya kuitumia.

Umiliki wa domain, hosting accounts, website files, licences na access utakubaliwa kwa maandishi. Mabadiliko yanayopanua scope yatajadiliwa kabla ya kutekelezwa.

05 / KABLA YA KUANZA

Maswali Na Majibu

Sijui website yangu inahitaji nini.

Hakuna shida. Tuambie kuhusu biashara yako na unachotaka website ikusaidie kufanya. Ukichagua “Nahitaji ushauri”, tutakusaidia kufafanua mahitaji kabla ya kuandaa quotation.

Sina logo, maandishi au picha zote.

Tuambie ulivyonavyo na unavyohitaji kusaidiwa. Gharama za kuandika maandishi, kutengeneza logo au kupiga picha zitajadiliwa kando.

Website itagharimu kiasi gani?

Tutakupa bei baada ya kujua kurasa, features na maandalizi yanayohitajika. Utapata maelezo ya kazi na gharama kabla ya kuamua kuendelea.

Itachukua muda gani?

Muda utategemea ukubwa wa kazi na kama maandishi na picha viko tayari. Tuambie tarehe unayolenga ili tuangalie kama tunaweza kuifikia.

Mnafanya booking, orders au malipo?

Tuambie unahitaji mfumo ufanye nini na kama una huduma nyingine unayotumia tayari. Tutaangalia kinachowezekana na kukueleza gharama kabla ya kuanza.

Website itaniletea mauzo moja kwa moja?

Website humsaidia mteja kuijua biashara na kukufikia. Ili kupata mauzo, bado unahitaji kuifikisha kwa watu sahihi na kujibu wanaoulizia. Hatuahidi idadi ya mauzo au nafasi fulani Google.

Nini kinatokea nikikamilisha questionnaire?

Utaona muhtasari wa majibu yako. Kisha unaweza kuutuma kwa WhatsApp au email, au kuunakili. Hatuupokei mpaka uutume kutoka kwenye app yako.

06 / TUANZE NA BIASHARA YAKO

Pata Quotation Ya Mradi Wako

Jibu maswali haya kuhusu website unayohitaji. Tutapitia majibu yako na kuwasiliana nawe kuhusu kazi, gharama na muda.

Bado hujajua kila kitu unachohitaji? Chagua “Nahitaji ushauri” pale inapofaa, au tuandikie WhatsApp.

Tuambie Unachohitaji

Biashara Yako

Majibu yanabaki kwenye ukurasa huu hadi uchague njia ya kutuma. Draft inaweza kuhifadhiwa kwenye tab hii kwa dakika 30 ili urudi bila kuanza upya. Kufunga tab huiondoa.

Soma maelezo ya faragha
HATUA INAYOFUATA

Kagua Ombi. Chagua Njia Ya Kutuma.

Pitia maelezo yako hapa chini. Ukiwa tayari, fungua WhatsApp au email na utume ujumbe. Bado hatujapokea ombi hili.

Endelea WhatsAppFungua email